Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kilichotokea Srebrenica yalikuwa mauaji mabaya zaidi Ulaya tangu Vita Kuu ya Pili ya dunia:Guterres

Kilichotokea Srebrenica yalikuwa mauaji mabaya zaidi Ulaya tangu Vita Kuu ya Pili ya dunia:Guterres

Pakua

Kuelekea kumbukumbu ya miaka 25 ya mauaji ya kimbari yaliyofanyika huko Srebrenica,Bosnia na Herzegovina, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema huo ulikuwa ukatili mbaya zaidi kufanyika katika ardhi ya Ulaya tangu Vita Kuu ya Pili ya Dunia. Taarifa zaidi na Jason Nyakundi.

Kupitia ujumbe maalum wa kumbukumbu hiyo ambayo kila mwaka hufanyika Julai 11, Antonio Guterres amesema miaka 25 baada ya mauaji hayo ya kimbari  ya 1995 Umoja wa Mataifa unawaenzi maelfu ya watu waliouawa kikatili na kuahidi kutowasahau asilani.

Guterres ameongeza kuwa Umoja wa Mataifa unashiriki majonzi ya familia nyingi zilizopoteza wapendwa wao ikiwemo wale ambao hadi sasa ndugu zao hawajapatikana na kuwahakikishia mshikamano manusura, robo karne iliyopita Umoja wa Mataifa na jumuiya ya kimataifa iliwaangusha watu wa Srebrenica na kama alivyosema Katibu Mkuu wa zamani Kofi Annan kuwaangusha huko kutaisakama historia yetu daima. Kukabiliana na historia hiyo ni hatu muhimu katika kuelekea kurejesha imani. Na maridhiano ni lazima yazingatie huruma na uelewa wa pande zote.”

Amefafanua kuwa maridhiano hayo ni kukataa hali ya kutokubali kuwa yaliyofanyika yalikuwa ni mauaji ya kimbari na uhalifu wa vita na juhudi zozote za kuwatukuza wahalifu wa vita waliohukumiwa.

Pia inamaanisha ni kutambua mateso ya waathirika wote na kutoonyesha hatia ya pamoja. Na kwa mantiki hiyo Guterres amesema“ndio sababu natoa wito kwa kila mtu kwenye ukanda huo na zaidi, kupambana na kauli za chuki, mtazamo wa migawanyiko na simulizi za kutoaminiana na kutia hofu. Jamii zote, viongozi wote na mashirika yote ikiwemo vyombo vya Habari lazima viweke ahadi hii. Raia wote wa Bosnia na Herzegovina wanastahili ahadi thabiti kutoka kwa viongozi wao , kushirikiana katika kuelekea mazingira ya kuheshimiana bila ubaguzi, chuki au uchochezi wa machafuko.”

Guterres amesema kumbukumbu hii ya majonzi ni kumbusho kwamba amani Bosnia na Herzegovina bado ni tete hivyo lazima kazi ifanyike kuelekea maridhiano ya kweli kwani hilo ni deni kwa waathirika wa mauaji ya kimbari ya Srebrenica, manusura, watu wote wa Bosnia na Herzegovina na binadamu wote.

 

Audio Credit
Anold Kayanda/Jason Nyakundi
Audio Duration
2'23"
Photo Credit
UNICEF/Roger LeMoyne