Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Mashariki ya Kati

Familia ya kipalestina ikiwa inaondoka eneo la Rafah, kusini mwa Ukanda wa Gaza
© UNICEF/Eyad El Baba

UNRWA: Waliokimbia Rafah wafikia 800,000

Kwa mara nyingine tena karibu nusu ya wananchi wote waliokuwa Rafah au watu 800,000 hivi sasa wapo njiani wakilikimbia eneo hilo ambalo lilianza kushambuliwa na jeshi la Israel Mei 6 mwaka huu baada ya kutolewa kwa amri na jeshi la Israel la kuwataka watu wote kuondoka eneo hilo.