Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WFP: Malori 10 ya msaada yawasili Gaza

Malori yanasafirisha chakula cha msaada hadi kaskazini mwa Gaza wakati wa mapumziko ya hivi majuzi ya kibinadamu.
© WFP/Ali Jadallah
Malori yanasafirisha chakula cha msaada hadi kaskazini mwa Gaza wakati wa mapumziko ya hivi majuzi ya kibinadamu.

WFP: Malori 10 ya msaada yawasili Gaza

Msaada wa Kibinadamu

Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP hii leo jumamosi limethibitisha kuwa malori yake 10 ya chakula yamesafirishwa na kuwasili Gaza katika ghala lake hapo jana kupitia gati mpya iliyojengwa. 

 

Baadhi ya bidhaa zilizomo ndani ya shehena hiyo iliyowasili Gaza ni pamoja na biskuti za kuupa mwili nguvu kutoka WFP ambazo watazisambaza kwa wananchi wa Gaza. 

Shehena hiyo pia ina bidhaa nyingine za wadau wa masuala ya kibinadamu ambao nao wanatarajia kuzisambaza kwa wapalestina ikiwemo mchele, tambi na mbaazi. 

Tayari WFP imekwisha waarifu wadau wake juu ya kuwasili kwa bidhaa hizo katika ghala lake lililopo eneo la Deir El Balah ili waweze kwenda kuzichukua na kusambaza kwa wahusika.