Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Heko Uganda kwa kuwaenzi wakimbizi:UNHCR

kamishina mkuu wa UNHCR Filipo Grandi akiwasikiliza wakimbizi kutoka Sudan Kusini wakati wa ziara yake nchini Uganda .

Heko Uganda kwa kuwaenzi wakimbizi:UNHCR

dailynews023c-18_01Kamishina mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR, ameipongeza  serikali ya Uganda kwa sera nzuri isiyokuwa na mipaka wala  urasimu inayowaenzi na kuwathamini  wakimbizi wanaoingia nchini humo. Tupate maeelezo kamili na Joseph Msami

Akiwa ziarani nchini Uganda,kamishina Filopo Grandi  akizungumza na wandishi wa habari, amesema Uganda ni nchi pekee Afrika  na hata duniani iliyo na sera nzuri zisizobagua wakimbizi kwenye mipaka yake na ni nchi pekee iliyotoa hifadhi kwa zaidi ya wakimbizi milioni 1.4.
(SAUTI YA FILIPPO GRANDI)
“Napenda kuchukua fursa hii kuishukuru, Serikali ya Uganda, sana sana na wananchi wa eneo hili kwa  kuendelea kuwapokea wakimbizi. Uganda inapokea zaidi ya wakimbi 500 kwa siku, wengi wao wakitoka Sudan Kusini na Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo na ukanda wa madharibi. Wengi wanakuja Uganda kwasababu ya sera nzuri na mapokezi mazuri ya serikali ya Uganda.
kwa sasa kambi za Impvepi na Rhino  zilizopo katika  wilaya ya Arua kuna takribani wakimbizi 245, 000 wengi wao wakitoka Sudani Kusini na kupewa hifadhi na ardhi kwajili ya kilimo na shughuli zingine za maendeleo.
Aidha bwana Grandi ametoa wito kwa serikali ya Uganda kuendelea  na sera hiyo ambayo huleta maendeleo katika sekta ya kilimo, miundombinu na pia ajira  kwa wenyeji  .
Katika ziara yake mkuu huyo wa UNHCR alikutanda na waziri mkuu wa Uganda Bwana Ruhakana Rugunda na kutoa shukrani kwa niamba ya Umoja wa Mataifa na kuahidi ushirikiano zaidi baina ya UNHCR na serikali ya Uganda katika kutafutia mwafaka swala la huduma kwa  ukimbizi katika eneo la maziwa makuu.