Maelfu ya raia wa DRC wamiminika Burundi

Maelfu ya raia wa DRC wamiminika Burundi

dailynews023a-18

Idadi ya wakimbizi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC waliongia nchini Burundi katika kipindi kisichozidi wiki moja imefikia zaidi ya Elfu 10.

Raia hao wamesaka hifadhi kwenye mikoa ya Rumonge na Makamba iliyoko kusini mwa Burundi na wengi wao wanatokea eneo la Fizi  mkoa wa Kivu kusini.

Wakimbizi hao wakiwa na watoto wengine wenye umri wa wiki mbili wamesema wanakimbia mapigano kati ya serikali na waasi wa MaiMai.

Kutoka Bujumbura mwandishi wetu wa Maziwa Makuu Ramadhani Kibuga ametuma ripoti hii.