Kongamano la kimataifa la takwimu na uhamiaji lang’oa nanga Paris:IOM
Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji IOM kwa ushirikiano na idara ya mambo ya uchumi na kijamii ya Umoja wa Mataifa UNDESA na shirika la ushirikiano wa maendeleo na uchumi OECD leo wameanza kongamano mjini Paris Ufaransa kuhusu ukusanyaji takwimu za uhamiaji duniani. Tupate tarifa zaidi na Patrick Newman
(TAARIFA YA PATRICK)
Kongamano hilo la siku mbili, lilofungiliwa na bwana Wiliam Lacy ni mkurugenzi mkuu wa IOM, Liu Zhenmin, katibu mkuu wa UNDESA na bi Angel Gurria katibu mkuu wa shirika la ushirikiano wa maendeleo na uchumi OECD pia limewaleta pamoja zaidi ya watalamu 700 wa maswala ya kukusanya takwimu duniani, asasi za kiraia na watunga sera ili kujadili swala la uhamiaji ambalo kwa sasa ni jambo mtambuka katika kila pembe ya duniani.
Bwana Swing wa IOM amesema , bila kuwepo na takwimu zinazoaminika ni vigumu kuweka bayana será na miongozo itakayowezesha kukabiliana na tatitzo la uhamiaji duniani.
Kongamano hilo ltakalo jadili pia mtitazamo na maoni ya watu na wenyeji katika nchi zinazopokea wahamiaji limepangwa kufanyika mara mbili kwa mwaka, kwa ushirikiano na mashirika mbalimbali yakijumuisha shirika la kazi duniani ILO, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudmia wakimbizi UNHCR,shirika la Umoja wa Mataifa la uhalifu na madawa UNODC, Eurostat na tume ya Umoja wa Mataifa ya maendeleo ya uchumi barani Ulaya UNECE, kama jukwaa la kukusanya takwimu na pia kujadili mikakaki ya maswala la uhamiaji duniani.