Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Busara na uzoefu wa wazee na vijana ni muhimu kwa SDG:Guterres

Busara na uzoefu wa wazee na vijana ni muhimu kwa SDG:Guterres

Busara, uzoefu, ari na mawazo ya wazee na vijana ni muhimu katika kuhakikisha utimizaji wa malengo yote 17 ya maendeleo endelevu yaani SDG’s. Huo ni ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres, katika mwanzo wa siku ya mjadala wa rika mbalimbali wenye lengo la kuchagiza mchango muhimu wa wazee na vijana katika utekelezaji wa malengo hayo.

Katika majadiliano hayo yanayofanyika kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa hapa New York leo, katika ujumbe wake Guterres amesisitiza kwamba vijana na wazee

(SAUTI YA GUTERRES)

“Kwa pamoja mnaweza kusaidia kuvunja mzunguko wa umasikini ambao umedumu kwa vizazi na vizazi na kuibua mabadiliko ambayo yanakumbatiwa na vijazazi vijavyo. Umoja wa Mataifa umejidhatiti kufanya kazi nanyi kwa ajili ya mustakhbali wa amani zaidi, wenye haki na mafanikio kwa wote.”

Naye mwakilishi maalumu wa vijana kwenye Umoja wa Mataifa Jayathma Wickramanayake akizungumza kwenye ufunguzi wa majadiliano hayo amesema

(SAUTI YA JAYATHMA)

“Majadiliano ya rika mbalimbali ni kipendee muhimu sana katika kufikia malengo ya maendeleo endelevu na kudumisha amani kwa wote, kujenga madaraja kwa ajili ya vizazi tofauti kuafanya kazi pamoja katika uhusiano wa kuwezeshana. Pia ni muhimu kutambua kwamba mkakati wa Madrid wa kuchukua hatua dhidi ya uzee ni kuwatoa wazee katika hali ya kutengwa, kuwajumuisha na kuwashirikisha na hivyo kuchagiza mshikamano miongoni kwa vizazi na kupambana na ubaguzi kwa misingi ya rika, uwezo na kujenga jamii ya rika zote.”