Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR yaomba dola milioni 9.5 kusaidia watu Kaskazini Mashariki mwa Nigeria

UNHCR yaomba dola milioni 9.5 kusaidia watu Kaskazini Mashariki mwa Nigeria

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limezindua ombi la msaada kwa ajili ya kuongeza shughuli zake Kaskazini Mashariki mwa Nigeria.

Shirika hilo linasema linahitaji dola milioni 9.5 zaidi kwa sababu ya kujerea kusikotarajiwa kwa wakimbizi wa Nigeria tangu mwanzo wa mwaka na wengi wa wakimbizi hao wanarejea kutoka Cameroon.

Kwa mujibu wa Volker Türk kamishina msaidizi wa masuala ya ulinzi kwa wakimbizi kwenye shirika la UNHCR, “ni lazima tufanye kila tuwezalo kuwasaidia watu hawa wasiojiweza

Ameongeza kuwa watu wengi wanaorejea hawawezi kwenda tena kwenye nyumba zao kutokana na hofu ya kiusalama , na wanaishia kutawanywa tena , katika hali ngumu ya kibinadamu.