Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

FAO kuanzisha mpango mpya kupima uwezekano wa kutokea njaa

FAO kuanzisha mpango mpya kupima uwezekano wa kutokea njaa

Shirika la Chakula na Kilimo duniani FAO lipo mbioni kufanya majaribio ya mpango mpya na wa haraka wa kupima tatizo la njaa na ukosefu wa usalama wa chakula.  Taarifa ya FAO inasema mpango huo ulipewa jina la hatua mpya-ya haraka na –ya uhakika, unatazamiwa kuanza kutekelezwa mwezi huu katika nchi za Angola, Ethiopia, Malawi na Niger kabla ya kusambazwa katika mataifa mengi zaidi.  Njia mojawapo inayotazamiwa kutumika ni pamoja na kukusanya taarifa kutoka kwa watu ambao wanakabiliwa mara kwa mara na matatizo ya chakula na kisha kuzifanyia uchambuzi wa kisayansi. Mkurugenzi msaidizi wa FAO katika masuala ya maendeleo ya uchumi na kijamii Jomo Sundaram, amesema kuwa nchi hizo nne zimekubali kwa pamoja kuendesha mipango itayosaidia kutokomeza tatizo la njaa ikiwa sehemu pia ya kuitikia mwito wa Katibu Mkuu Ban Ki-moon aliyetangaza kampeni ya kutokomeza njaa duniani kote.