Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Teknolojia yaweza kusaidia maendeleo kwa amani na utu-Guterres

Teknolojia yaweza kusaidia maendeleo kwa amani na utu-Guterres

Wadau wakuu wa uwezo wa masuala ya teknolojia AI na wale wa mambo ya kibinadamu wanakutana na viongozi wa viwanda na taaluma katika mkutano wa kimataifa uliopewa jina Yote kwa wema.

Mkutano huo unafanyika mjini Geneva, Uswisi, ambapo mjadala unahusu namna AI inavyoweza kusaidia juhudi za kukabili umasikini, njaa na kuwezesha elimu na afya pamoja na ulinzi wa mazingira.

Akizungmzia umuhimu wa mkutano huo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres, amesema teknolojia ina umuhimu katika kukuza maendeleo kwa kuzingatia utu, amani, na mafanikio kwa watu wote.

Kuhusu nchi zinazoendelea amesema na teknolojia amesema.

( Sauti Guterres)

"Nchi zinazoendelea zaweza kunufaika kupitia teknolojia lakini pia zinakabiliwa na hatari ya kuachwa nyuma. Mkutano huu waweza kusaidia kuhakikisha teknolojia inanufaisha wanadamu wote na kufanikisha malengo yetu ya pamoja"

Shirika la Umoja wa Mataifa la teknolojia ya taarifa na mawasiliano ITU, ndilo linaloratibu mkutano huo pamoaj taasisi ya XPRIZE na wadau wengine 20, ambapo washiriki kutoka kutoka kampuni kuu zaidi ya 70 na taasisi za kitaaluma na utafiti watahudhuria.