Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Upinzani dhidi ya haki za wanawake hutuathiri sote- Zeid

Upinzani dhidi ya haki za wanawake hutuathiri sote- Zeid

Inasikitisha sana kuona mafanikio yaliyopatikana kuhusu haki za wanawake, yaanza kurudishwa nyuma katika baadhi ya maeneo duniani, amesema Kamishna Mkuu wa haki za binadamu Zeid Ra’ad Al Hussein katika ujumbe wake kuelekea siku ya wanawake duniani siku ya Jumatano. Rosemary Musumba na ripoti kamili.

(Taarifa ya Rosemary)

Kamishna Zeid amesema mamilioni ya wanawake walijitoa maisha yao ili kunasua siyo tu haki zao bali pia za wanawake wenzao, jambo lililoleta mabadiliko makubwa chanya, ingawa kwingineko kwa kasi ndogo.

Hata hivyo amesema kinachosikitisha sasa baadhi ya nchi zinarudisha nyuma maendeleo hayo kwa kupitisha sheria za kudhibiti uamuzi wa mwanamke juu ya familia yake na hata mwili wake kwa muktadha kwamba jukumu la mwanamke ni kuzaa watoto na kulea familia.

Amesema ajenda hizo ambao mara nyingi zinatekelezwa kwa kisingizio cha utamaduni zinatekelezwa kwa lengo la kuleta mabadiliko huku zikitishia mafanikio yaliyopatikana kuhusu haki za wanawake na kuathiri jamii nzima.