Usawa wa kijinsia ni suluhu ya 50/50 ifikapo 2030- UM
Ikiwa leo ni siku ya wanawake duniani ujumbe ukiangazia wanawake katika mazingira yanayobadilika ya kazi, kuelekea usawa wa kijinsia mwaka 2030, Umoja wa Mataifa umetaka ushiriki wa wanawake kikamilifu ili kufanikisha azma hiyo. Assumpta Massoi.
(Taarifa ya Assumpta)
Nats..
Kibao hicho I will rise up kiliporomoshwa na mwimbaji mwenye kipaji Jana Brown kwenye moja ya kumbi za Umoja wa Mataifa, makao makuu jijini New York… mbele ya viongozi mbali mbali wakiwemo wadau wa masuala ya wanawake..rangi nyekundu ikitawala! akimaanisha na nitanyanyuka kwa ajili yangu na ajili yako!
Nats..

Naye Mwenyeji wa tukio hili, Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Umoja wa Mataifa kuhusu wanawake, UNWomen, Phumzile Mlambo-Ngucka awali alipigia chepuo sera za ajira zinazozingatia usawa wa kijinsia akisema..
(Sauti ya Phumzile)
"Mathalani kwenye tasnia ya ukaguzi, Ernst & Young imeonyesha kuwa iwapo ukituma kwa mteja wako timu ya ukaguzi yenye usawa wa kijinsia unamwacha mteja wako akiwa ameridhika. Na katika sekta nyingi na viwandani ubora wa uamuzi unaimarika pindi unapokuwa na timu jumuishi na siyo wanawake tu,bali pia watu wenye ulemavu, na makundi madogo."
Nats..