Skip to main content

Chuja:

Siku ya Wanawake 2017

Kilimo cha buni chastawisha maisha ya wanawake Uganda.

Ujasiriamali ni miongoni mwa mikakati bunifu ya kuwawezesha wanawake kuinuka kiuchumi wakati huu ambapo malengo ya maendeleo endelevu SDGs yanapigia chepuo uwezeshaji wa wanawake katika kila ngazi.

Nchini Uganda, licha ya changamoto kadhaa, Betty ni mfano wa wanawake waliofanikiwa kupitia kilimo cha mibuni. Ungana na John Kibego katika makala ya kumulika mafaniko ya mwanamke huyo.

Wakimbizi Kigoma waadhiimisha siku ya wanawake

Maadhimisho ya siku ya wanawake nchini Tanzania yamefanyika sehemu mbalimbali licha ya kwamba kitaifa yamefanyika mkoani Singida.

Mkoani Kigoma katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu, mvua kubwa iliyonyesha awali haikuwazuai wananchi kujitokeza kuhudhuria maadhimisho hayo yaliyotia fora kwa burudani na ujumbe. Tuungane na Mabamba Mpela Junior

Kuelekea 2030, wanawake wamejizatiti kufikia #5050

Tarehe Nane mwezi Machi, kwa zaidi ya karne moja sasa, imekuwa ni siku  ya kuadhimisha siku ya wanawake duniani. Siku hii ikiangazia harakati za kuweka usawa wa kijinsia kwa mustakhbali bora siyo tu wa kundi hilo ambalo ni zaidi ya asilimia 50 duniani, bali pia kwa ulimwengu wote kwani wahenga walisema ukimwendeleza mwanamke umeendeleza jamii nzima.

Sasa katika maadhimisho haya tumetathmini hali ya mwanamke kiuchumi, kisiasa na kijamii na mwelekeo wa usawa wa 50 kwa 50 ifikapo mwaka 2030 katika mazingira ya sasa ya kazi ulimwenguni yanayobadilika.

Burudani zasheheni wakati wa kuadhimisha siku ya wanawake duniani.

Wanawake wameshamiri juma hili. Mataifa mengi yameadhimisha siku ya wanawake duniani mnamo Machi nane, siku ambayo huadhimishwa kila mwaka, lengo likiwa kupigia chepuo haki na ustawi wa kundi hilo katika nyanja mbalimbali.

Katika makala ifuatayo Assumpta Massoi anamulika namna burudani ilivyotumiwa kufikisha ujumbe hususani nchi zenye mizozo, huku ikiwaliwaza washiriki, wakiongozwa na wanawake ambao ni walengwa.

Tukipata teknolojia wezeshi tutazalisha maradufu: Wajasiriamali Wanawake

Ukosefu wa teknolojia wezeshi unapunguza mapato kusudiwa kwa wanawake mkoani Kagera nchini Tanzania, hii ni kwa mujibu wa wajasiriamali mkoani humo ambao wanasema wakiwezeshwa kiteknolojia watazalisha maradufu.

Nicolaus Ngaiza wa redio washirika Kasibante Fm ya Kagera nchini humo, amevinjari hadi wajasiriamali hao wanawake wanapofanya kazi zao ili kujionea. Ungana naye katika makala ifuatayo.