Kutokuzingatia haki za binadamu ni ugonjwa: Guterres
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema huu ni wakati wa dharura na tume ya uchunguzi na ujumbe wa haki za binadamu hutafuta ukweli kwa sababu ya madai makubwa ya ukiukwaji wa haki za binadamu kote duniani. Flora Nducha na taarifa kamili
(TAARIFA YA FLORA)
Bwana Guterres amesema hayo hii leo katika ufunguzi wa kikao cha 34 cha Baraza la Haki za binadamu kilichoanza mjini Geneva, Uswis.
Ameongeza kuwa
(Sauti ya Guterres)
"Kutokuzingatia haki za binadamu ni ugonjwa, ugonjwa ambao unaenea - kaskazini, kusini, mashariki na magharibi. Baraza la Haki za Binadamu lazima kuwa sehemu ya tiba."
Amesema uchunguzi na mapendekezo ya wataalam huru hutoa mwangaza ili kuimarisha ulinzi na sera za mwongozo. Na kwamba licha ya tofauti miongoni mwa wanachama, amelitaja baraza kuwa ni misingi wa uelewa kwa pamoja, kushikilia haki za watu wote na kwa maslahi ya nchi zote.

(Sauti ya Zeid)
"Jumuiya ya kimataifa haiwezi kunyamaza na kukaa kando kwa kuwa kuna mengi ya kupoteza na mengi ya kulinda. Haki za wote na kutetea dunia yetu haipaswi kuwekwa kando na wale wanaotaka kujinufaisha kisiasa"
Zeid amesema kuwa Ofisi yake inafanya kazi na taasisi za kikanda na kitaifa na asasi za kiraia katika ngazi zote ili kukuza na kulinda haki za binadamu kwa watu wote na kila mahali.