Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNESCO yatumia meli kupigia chepuo nishati endelevu

UNESCO yatumia meli kupigia chepuo nishati endelevu

Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduani, UNESCO linashiriki katika mradi wa meli ya kwanza duniani isiyotumia nishati ya kisukuku au mafuta yanayotoa hewa ya ukaa kama njia ya kupigia chepuo nishati endelevu.

UNESCO kupitia taarifa yake imesema meli hiyo Energy Observer inazalisha nishati yake yenyewe kwa kutumia maji ya bahari na hatimaye nishati hiyo inahifadhiwa kwenye meli.

Lengo la mradi huo ni kupigia chepuo matumizi ya nishati mbadala huku ikiangazia changamoto za nishati endelevu.

Meli hiyo itatia nanga katika maeneo 101 ikiwemo miji mikuu ya bandari, bandari za kihistoria, hifadhi ya maliasili au matukio makubwa ya kimataifa.

Yaelezwa kuwa meli hiyo Energy Observer itafanya safari kwa miaka sita bila kutumia nishati ya kisukuku.