Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uwekezaji wa nje kimataifa uliyumba 2017: UNCTAD

Ripoti ya uwekezaji wa nje. Picha: UNCTAD

Uwekezaji wa nje kimataifa uliyumba 2017: UNCTAD

Ukuaji wa Kiuchumi

Uwekezaji wa kimataifa wa moja kwa moja toka nje (FDI) uliporomoka kwa asilimia 16 mwaka 2017 na kufikia dola trition 1.52 kutoak dola trilioni 1.81 mwaka 2016, imesema leo ripoti ya mwenendo wa uwekezaji kimataifa iliyotolewa na kamati ya Umoja wa Mataifa ya maendeleo na biashara UNCTAD.

Kwa mujibu wa Mukhisa Kituyi Katibu Mkuu wa UNCTAD, uwekezaji wa kimataifa wa moja kwa moja toka nje unaendelewa kukabiliwa na changamoto huku katika mataifa yanayoendelea kukiwa hakuna mabadiliko makubwa na miaka ya nyuma, na uwekezaji zaidi katika sekta zitakazochangia katika maendeleo endelevu au SDG’s unahitajika sana.

Ameongeza kuwa kuchagiza FDI kwa ajili ya utimizaji wa SDG’s bado ni changamoto kubwa na chanzo kikubwa cha kuporomoka huko ni ukuaji wa asilimia 11% wa uwekezaji kwa nchi zinazoendelea, hasa Australia.

Ripoti hiyo  inasema uwekezaji kwa nchi zinazoendelea bado ni imara ukiingiza dola bilioni 653 mwaka 2017 ikiwa ni ongezeko la asilimia 2% ikilinganishwa na 2016. Ongezeko hilo limedhihirika kwa nchi za Asia, Amerika ya Kusini na Caribbean wakati barani Afrika Hakuna mabadiliko.

Kwa mujibu wa ripoti ya UNCTAD kushuka kwa uwekezaji hakujaathiri pato la taifa au kukua kwa biashara ambayo ilipanda 2017.

Mwaka 2018 unatarajiwa ukuaji wa uchumi, biashara na pia kupanda kwa kiwango cha FDI.