Msaada toka EU wanusuru maelfu ya wakimbizi: WFP

28 Disemba 2016

Shirika la mpango  wa chakula duniani WFP, limekaribisha kuendelea kwa usaidizi kati ya Muungano wa Ulaya EU na shirika hilo ambapo wakimbizi na wasaka hifadhi 17,000 nchini Djibouti wamenufaika.

Taarifa ya WFP inasema kwamba wakimbizi hao wamepatiwa fedha tasilimu pamoja na mgao wa chakula .

WFP imeongeza pia kuwa fedha kutoka kamisheni ya Ulaya ya msaada wa kibinadamu na idara ya ulinzi wa raia (ECHO) zimewezesha shirika hilo kutoa fedha taslimu kwa wakimbizi 13,000 kutoka Somalia, Ethiopia na Eritrea.

Pia msaada wa kifedha wa nyongeza uliotolewa mwishoni mwa mwaka, uliwezesha WFP kutoa  msaada kwa wasaka hifadhi 4,000 waliowasili hivi karibuni nchini Ethiopia.

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter