Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanaojitolea wanajenga hamasa: Ban

Wanaojitolea wanajenga hamasa: Ban

Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya kujitolea, Umoja wa Mataifa umesema kundi la wanaojitolea ni chombo muhimu kwa mustakabali wa sayari dunia.

Hiyo ni sehemu ya ujumbe wa Katibu Mkuu wa umoja huo Ban Ki-moon kuhusu siku hiyo ambapo amesema anatuma salamu zake za pongezi kwa zaidi ya watu 6000 wa Umoja wa Mataifa wanaojitolea, wengine 12,000 wanojitolea kupitia mtandao na zaidi ya bilioni moja wanaojitolea katika jamii duniani.

Amesema wajibu wao na kujituma ni hamasa kwa dunia kwa ujumla.

Ban ametaka jamii kuitumia siku hii kutambua umuhimu wa watu wanaojitolea wakati wakitekeleza wajibu huo, kuwapongeza kwa uraia wao wa kimataifa katika kujenga mustakabali wa amani, mafanikio na utu kwa wote.