Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hatua madhubuti zahitajika Ulaya kwa ajili ya wakimbizi: UNHCR

Hatua madhubuti zahitajika Ulaya kwa ajili ya wakimbizi: UNHCR

Wito umetolewa Jumatatu na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumiwa wakimbizi UNHCR, likiutaka Muungano wa Ulaya kufanyia mabadiliko mfumo wake wa kimataifa wa kushughulikia wakimbizi na waomba hifadhi.

Kwa mijibu wa Filippo Grandi Kamisha mkuu wa UNHCR, wameitaka Ulaya kutoa usaidizi wa kimtakati zaidi kwa walengwa kwenye nchi za asili, hifadhi na makazi ya muda kwa wakimbizi.

Pia wameitaka Ulaya kutathimini maandalizi ya dharura ili kukabiliana na wimbi kubwa la wakimbizi na wahamiaji wanaowasili na kuweka mfumo bora na wenye ufanisi zaidi wa kushughulikia waomba hifadhi.

UNHCR pia imeomba kuwepo na uwekezaji mkubwa wa nchi wanachama wa EU katika ushirikiano wa masuala ya wakimbizi,ukijumuisha masuala ya makazi, ajira na mafunzo lugha.