Skip to main content

Watu milioni 18.2 sasa wanapata dawa za kupunguza makali ya ukimwi: UNAIDS

Watu milioni 18.2 sasa wanapata dawa za kupunguza makali ya ukimwi: UNAIDS

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya ukimwi UNAIDS limetangaza kwamba watu milioni 18.2 kote duniani sasa wanapata dawa za kupunguza makali ya ukimwi. Flora Nducha na taarifa kamili

(TAARIFA YA FLORA)

Kwa mujibu wa ripoti mpya ya shirika hilo iitwayo”Pata huduma ya haraka:mzunguko wa maisha na mtazamo wa HIV, iliyozinduliwa Jumatatu Windhook Namibia, nchi nyingi sasa zinapata huduma ya haraka huku kukiwa na ongezeko la watu milioni moja wanaopata dawa hizo katika miezi sita iliyopita kuanzia Januari hadi Juni 2016. Watu zaidi ya milioni 18 sasa wanapata dawa za kupunguma makali wwakiwemo watoto 910,000.

Hata hivyo shirika hilo limeonya kwamba vijana walio na umri wa kati ya miaka 15-24 wako kwenye hatari zaidi ya kuambukizwa virusi vya HIV hususani wasichana walio Afrika Kusini mwa jangwa la Sahara na kutoa wito wa kuchukua mtazamo mpya kuwanusuru. Naibu mkurugenzi mkuu wa UNAIDS ni Luiz Loures anasema pamoja na mafanikio kuna changamoto

(SAUTI YA LUIZ LOURES)

"Changamoto ni kuhakikisha hatua zinapigwa katika tiba, tunahitaji kuwenda na kasi hiyohiyo katika kuzuia, tunahitaji kubadilika, na kufanya vizuri hasa kwa kuzia maambukizi ya HIV kwa vijana, tunahitaji kutumia vmitandao ya kijamii na kuwashirikisha vijana msitari wa mbele sio tu kama wapokea ujumbe bali kusaidia”