UNTWO, Kenya kukuza ajira za utalii.

UNTWO, Kenya kukuza ajira za utalii.

Shirika la Umoja wa Mataifa la utalii UNTWO linashirikiana na serikali ya Kenya katika kuongeza ajira kwenye sekta ya utalii.

Hatua hiyo imefikiwa kupitia utiliwaji wa saini wa makubaliano ya kutoa ajira kwa vijana na wanawake wa jamii zilikosa fursa za ajira na ujasiriamali katika utalii.

Kwa mujibu wa makubalianao hayo mpango wa mfano utazinduliwa nchini Kenya kabla ya mwisho wa mwaka 2017 na utajumuisha jamii za mitaa kupitia mpango uitwao Amadeus ambao ni kampuni ya kusongesha taklenlojia katika masuala ya utalii.

Juhudi hizo zinatarajiwa kuigwa dunaini kote, imesema taarifa hiyo.