Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WMO yanoa wawasilishaji wa utabiri wa hali ya hewa

WMO yanoa wawasilishaji wa utabiri wa hali ya hewa

Wakati mkutano wa 22 wa nchi wanachama wa mkataba wa mabadiliko ya tabianchi COP22 ukiendelea huko Marrakesh, Morocco, shirika la hali ya hewa duniani WMO, linawafundisha watangazaji wa vipindi vya utabiri wa hali ya hewa katika vyombo vya habari hususani nchi zinazoendelea kuhusu namna bora ya kuwasilisha ujumbe kuhusu mabadiliko hayo kwa hadhira.

Katika mahojiano na redio ya UM kutoka Marrakech, mwezeshaji Jill Peeters ambaye ni mbobezi katika masuala ya hali ya hewa na mwasilishaji wa masuala hayo runingani nchini Ubelgiji, amesema wawasilishaji wa utabiri wa hali ya hewa sasa wanawajibu wa zaidi ya kile wanachokifanya hivi sasa wanapowasilisha utabiri wa hali ya hewa.

(SAUTI JILL)

‘‘Sisi ni kama gundi,na gundi haionekani kama muhimu sana, lakini kama hakuna gundi huwezi kushikamanisha vitu, nina matumaini kwamba baada ya warsha hii hata wanasiasa watatutizama kama wawasilishaji wazuri na kwa pamoja tunaweza kuwezesha hatua hii ya dharura.’’

Amesema iamani liyonayo hadhira kwa wawasilishaji wa utabiri wa hali hewa ikitumiwa vizuri yaweza kusaida katika elimu ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.