Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

COP22

"Enzi mpya ya utekelezaji na hatua" kuhusu mabadiliko ya tabia nchi:COP22

Nchi zilizokusanyika kwenye mkutano wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabia au COP22 , zimetangaza tamko la “enzi mpya ya utekelezaji na hatua kuhusu mabadiliko ya tabia nchi.”Tamko la hatua la Marrakech, limetolewa leo Ijumaa siku ya mwisho ya mkutano huo uliokunja jamvi nchini Morocco, likisema, jumuiya ya kimataifa ina wajibu wa haraka wa kuchukua hatua dhidi ya dunia inayozidi kuchemka , ili kuhakikisha kiwango cha joto kinasalia chini ya nyuzi joto 2 celsius.

Afrika kufaidika kwanza na mfumo wa tahadhari ya majanga:COP22

Nchi za Afrika zenye maendeleo dunia na visiwa vya Pacific watakuwa wa kwanza kufaidika na mfumo ulioboreshwa wa tahadhari dhidi ya hali ya hewa na athari zinazohusiana na mabadiliko ya tabia nchi kupitia mkakati wa kuchukua hatua ulioainishwa na mkutano wa Umoja wa mataifa wa mabadiliko ya tabia nchi unaoendelea Morocco.

Nchi hizo zikiwemo Mali, Burkina Faso, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC nan chi za visiwa vidogo zinazoendelea , zitapatiwa msaada wa awali wa dola milioni 12 zilizotengwa na mradi wa athari za mabadiliko ya tabia nchi na tahadhari ya mapema (CREWS).