Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakuu wa nchi na serikali kujadili mabadiliko ya tabia nchi kuanzia Jumanne :COP22

Wakuu wa nchi na serikali kujadili mabadiliko ya tabia nchi kuanzia Jumanne :COP22

[caption id="attachment_300997" align="alignleft" width="300"]cop22africa

Siku 10 baada ya kuanza kutekelezwa mkataba wa Paris wa mabadiliko ya tabia nchi , wakuu wa nchi na serikali wanatarajiwa Jumanne ijayo kwenye mkutano wa Umoja wa Mataifa wa mbadiliko ya tabia nchi au COP22, ulioanza Novemba 7 mwaka huu mjini Marrakech, Morocco.

Kabla ya mkutano huo kukunja jamvi Novemba 18 nchi wanachama wanatumai kuweka sharia za mnkataba huo na kuainisha mipango madhubuti kwa kuchangia takribani dola bilioni 100 kwa mwaka kwa nchi zinazoendelea ili kusaidia hatua za kukabili mabadiliko ya tabia nchi.

Mkataba wa Paris ambao sasa umeridhiwa na nchi 105 una lengo la kuimarisha juhudi za kimataifa katika kukabiliana nan a tisho la mabadiliko ya tabia nchi kwa kuhakikisha wanadhibiti ongrezeko la joto duniani katika karne hii na kusalia kuwa chini ya nyuzi joto 2.

Mkutano wa COP22 hadi sasa umeshajadili mada mbalimbali ikiwemo misitu, maji, miji, nishati na usafiri, pia ukielezea umuhimu wa jukumu la sekta binafsi ikiwemo makampuni ya biashara, miji na mashirika yasiyo ya kiserikali yaani NGO’s katika utekelezaji wa mkataba wa Paris.