Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maendeleo yalinivunja moyo hadi ilipokuja ajenda ya 2030: Thomson

Maendeleo yalinivunja moyo hadi ilipokuja ajenda ya 2030: Thomson

Haraka ya kuondoka kijijini na kwenda kutafuta maisha mijini katika miaka ya 70 ilikuwa inamfanya Rais wa sasa wa baraza kuu la Umoja wa mataifa kuvunjika moyo.

Akizungumza kutokana na uzoefu wake mjini Quito Equador, Peter Thomson amesema miradi ya maendeleo vijijini ilikuwa ikipotea bure kutokana na kupungua kwa idadi ya watu katika nchi masikini, hadi ilipowasili ajenda ya 2030 ya maendeleo endelevu au SDG’s.

Hamasa yake kwa malengo hayo imedhihirika alipotemebea mradi mpya wa ubunifu kuhusu ukuaji wa miji iliyoonyeshwa kwenye mkutano wa makazi unaoendelea mjini Quito. Anafafanua ni kwa nini anaimani na ajenda mpya ya miji na umuhimu wake kwa maendeleo ya dunia

(SAUTI THOMSON)

“Kwa sababu malengo ya maendeleo endelevu ni kwa ajili ya mustakhbali wa kila mtu, watoto wao, wajukuu zao na watakaokuja baada yao, na ni kwa ajili ya kila nchi duniani, nimefanya kazi kwa miaka 10 kama afisa maendeleo vijijini, na maendeleo yalikuwa yananivuja moyo kwa sababu unawekeza katika masuala ya maji, usafi na ukimaliza kuweka barabara kila mtu ameshaondoka kwenda mjini. Hadi pale nilipoiona ajenda ya 2030 na malengo 17 ya maendeleo endelevu ndiopo nikatambua haya ndio maendeleo.”