Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mafanikio ya SDGs yanategemea mafanikio ya miji: Ban

Mafanikio ya SDGs yanategemea mafanikio ya miji: Ban

Ufikiaji wa malengo 17 ya maendeleo endelevu yaani SDG's utategemea kwa kiasi kikubwa endapo miji na makazi itajumuisha wote, itakuwa salama, inayohimi na endelevu. Amina Hassan na taarifa kamili

(Taarifa ya Amina)

Hayo ni kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon akizungumza katika ufunguzi wa mkutano wa tatu wa kimataifa kuhusu makazi, yaani HABITAT 111 mjini Quito Equador.

“Ajenda mpya kuhusu makazi na miji itakayopitishwa na mkutano huo itaweka viwango vya kimataifa vya maendeleo endelevu ya miji na kusaidia kufikiria upya jinsi ya kujenga, kudhibiti na kuishi mijini.”

Amesema maemeo ya mijini yanapanuka kwa haraka, hususani kwenye nchi zinazoendelea na ukuaji huo mara nyingi si wa mpango.

Inakadiriwa karibu robo ya wakazi wa mijini wanaishi katika mitaa ya mabanda na makazi yasiyo rasmi.