Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano wa HABITAT III kufunga pazia Quito

Mkutano wa HABITAT III kufunga pazia Quito

Mkutano wa tatu wa makazi yaani HABITAT III unakunja jamvi hii leo mjini Quito Ecuador. Mkutano huo unamalizika kwa nchi 193 wanachama wa Umoja wa Mataifa kupitisha ajenda mpya ya miji.

Ajenda hiyo inalenga kuwawezesha wakazi wote wa mijini wakiwemo wahamiaji na wakimbizi wawe wanaishi kwenye makazi rasmi ama yasiyo rasmi kuishi maisha bora, yenye hadi na yenye faid.

Mkutano huo umejadili masuala mbalimbali ikiwemo uhalifu mijini utokanao na ongezeko la watu wanaohamia mijini. Inakadiriwa kuwa barani Afrika pekee kutakuwa na watu milioni 900 zaidi watakaoishi mijini ifikapo mwaka 2050.

Juma Assiago ni mratibu wa mpango wa miji salama anasema wamejitahidi kukabiliana na uhalifu mijini

(SAUTI YA ASSIAGO)

Ameongeza kuwa changamoto ni fedha hasa kwa makundi mawili waathirika wakubwa

(SAUTI YA ASSIAGO)