Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mzozo ulioko bonde la ziwa Chad umesahaulika- Eliasson

Mzozo ulioko bonde la ziwa Chad umesahaulika- Eliasson

Raia wameuawa, nyumba zimetiwa moto, mali zimeporwa na mbinu za kujikwamua kimaisha zimesambaratishwa.

Hiyo ni taswira iliyoanikizwa na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Jan Eliasson wakati wa mkutano wa ngazi ya juu jijini New York, Marekani kuhusu mustakhbali wa nchi zilizopo bonde la ziwa Chad, ambalo wakazi wake zaidi ya Milioni Tisa wanahitaji misaada ya kibinadamu.

(Sauti ya Eliasson)

“Tusijesababisha mzozo katika bonde la mto Chad, ukawa janga lililosahaulika. Lazima tushirikiane na msingi wa harakati zetu uwe wananchi hao ambao wanahaha kusaka msaada kutoka kwetu.”

image
Rais Muhammad Buhari wa Nigeria aangazia suala la kibinadamu. Picha: BUHARI/JC McIlwaine
Rais Muhammad Buhari wa Nigeria akaangazia suala la kibinadamu akisema.

(Sauti ya Buhari)

“Ni lazima tuandae mfumo unaofanya kazi wa kusambaza misaada ili watoa misaada wote wasambaze misaada kwa umoja.”

Jumuiya ya nchi za kiislamu, OIC ambayo ni muaandaji mwenza wa kikao hicho iliwakilishwa na Katibu Mkuu Iyad Ameen Madani ambaye amesema pamoja na changamoto za usalama, zipo za mazingira zinazosababisha ziwa Chad kusinyaa hivyo..

(Sauti ya Iyad)

“Tunashirikiana na benki ya dunia na bila shaka benki ya maendeleo ya OIC na mamlaka ya hali ya hewa ya Saudi ili kutekeleza mradi wa kupunguza madhara ya majanga ndani ya nchi wanachama wa OIC ikiwemo eneo la bonde la Chad.”