Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mwaka Mmoja wa SDG’s mshikamano zaidi wahitajika kuyatekeleza

Mwaka Mmoja wa SDG’s mshikamano zaidi wahitajika kuyatekeleza

Ikiwa ni mwaka mmoja tangu kupitishwa malengo ya maendeleo endelevu SDG’s , zaidi ya nchi 50 tayari  zimeyafanya malengo hayo kuwa kuwa kitovu cha mipango yao ya maendeleo.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesisitiza kuwa, ili Kufikia malengo hayo, kuna  umuhimu wa kufuatilia ahadi hiyo ya mageuzi kwa maisha bora ya baadaye na ni lazima hatua zichukuliwe na kuwe na uwajibikaji.

Kenya ni miongoni mwa nchi ambazo zimeshikia bango utekelezaji wa malengo hayo ambapo makamu wa Rais wa nchi hiyo William Ruto anasema..

(SAUTI YA RUTO)

Nayo Somalia licha ya changamoto kubwa ya vita na wakimbizi imejizatiti kuhakikisha hakuna anayesalia nyuma kama anavyofafanua   Ahmed Said Farah mshauri wa kitaifa wa masuala ya wakimbizi na wakimbizi wa ndani Somalia

(SAUTI YA AHMED SAID FARAH)