Skip to main content

IAEA yaunda nyenzo za mafunzo ya nyuklia kwa nchi wanachama

IAEA yaunda nyenzo za mafunzo ya nyuklia kwa nchi wanachama

Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki (IAEA), limeunda nyenzo za kutoa mafunzo kwa nchi wanachama kuhusu jinsi ya kuanzisha na kuendesha programu za nishati ya nyuklia.

Kupitia nyenzo hizo za mafunzo zinazopatikana kwenye tovuti ya IAEA, wataalam na watunga sera sera katika nchi wanachama wataweza kupata mafunzo kutokana na uzoefu wa IAEA, ili waimarishe ufanisi na usalama wa matumizi ya nishati ya nyuklia, na kuzisaidia nchi wanachama kubadilishana ujuzi.

Kwa mujibu wa taarifa ya IAEA, kuunda mpango wa nyuklia ni kazi kubwa inayohitaji kupanga kwa umakini mkubwa, maandalizi, na uwekezaji katika taasisi na wataalam, na kunaweza kuchukua muda wa hata muongo mmoja.

Tayari, takriban watumiaji 7,400 kutoka nchi 50 zenye mipango ya nyuklia au zile zinazoianzisha, wameweza kutumia nyenzo hizo za mafunzo kupitia intaneti, ambazo zimekuwepo tangu mwaka 2013.