Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ni wakati wa kukomesha ukatili wa polisi dhidi ya raia-OHCHR

Ni wakati wa kukomesha ukatili wa polisi dhidi ya raia-OHCHR

Kikundi cha Wataalam wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa wameitaka serikali ya Kenya, mara moja kuzuia ukatili uanotendwa na polisi wa nchi hiyo na kuwajibisha wale wote waliohusika na mauaji yasiokubalika kisheria. John Kibego na taarifa saidi.

(Taarifa ya Kibego)

Watalamu hao wamepaza sauti wakati ambapo mafisa wa polisi wane wanakabiliwa na mashitaka ya kuua wakili wa haki za biandamu Willie Kimani, mteja wake Josephat Mwenda, na dereva wao, Joseph Muiruri, katika orodha ndefu ya mashitaka kuhusu kutoweka na mauaji nchini humo.

Wamesema, mauaji ya hivi karibuni ya wakili maarufu na mtetezi wa haki za binadamu yana atahri kubwa kwa mashirika ya kiraia hasa yale yalio shupavu katika utetezi wa haki za binaadamu, wakisisitiza kuwa ni lazima serikali ya Kenya ichukue hatua dhidi ya polisi wanaohusika na kupanga njama hizo za ukatili.

Ripoti iliyowasilishwa na Kamisheni ya Kitaifa ya Haki za binadamu kwa bunge la Kenya mwaka jana, ilionyesha ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu yakiwemo mauaji, utesaji na watu kukamatwa na kuzuiliwa kinyume cha sheria, ukihusisha mafisa wa polisi na vyombo vingine vya usalama.