Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNICEF yakaribisha ripoti inayopinga ukatili dhidi ya watoto

UNICEF yakaribisha ripoti inayopinga ukatili dhidi ya watoto

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto(UNICEF), limekaribisha ripoti inayopinga ukatili dhidi ya watoto, iliyotolewa na shirika linalofuatilia masuala ya haki za binadamu Human Rights Watch.

Kwa mujibu wa mkurugenzi wa UNICEF anyehusika na ulinzi kwa watoto Cornelius Williams, ripoti hiyo “hatua kali:ukatili dhidi ya watoto ni tishio la usalama wa taifa” inafafanua kuhusu ukiukwaji wa haki za watoto.

Bwana Williams amesema watoto ni lazima wahakikishiwe haki za kisheria na ulinzi ,bila kujali mashitaka yanayowakabili, na ni lazima walindwe na mfumo wa sheria za jinai.

UNICEF imezitaka serikali kutoa kipaumbele katika haki za watoto kwa kutekeleza mapendekezo yaliyotolewa na ripoti hiyo na kuzingatia viwango vya kimataifa vya haki kwa vijana.