Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNRWA yazindua wiki za michezo kwa watoto wakimbizi Gaza

UNRWA yazindua wiki za michezo kwa watoto wakimbizi Gaza

Shirika la Umoja wa Mataifa linalowasaidia wakimbizi wa Kipalestina, UNRWA, limezindua wiki za michezo na sanaa kwa watoto wakimbizi huko Gaza, kwa lengo la kutoa nafasi na mahali salama kwa watoto wakimbizi kufurahia maisha.

Kwa kipindi cha wiki tatu, watoto wakimbizi zaidi ya 165,000 waliosajiliwa watashiriki katika michezo hiyo katika maeneo 120 katika Ukanda wa Gaza, ikihusisha shule 108 na vituo vya mahitaji maalum.

Katika juhudi za kuendeleza maadili ya kijamii ya uongozi, heshima na ushirikiano, watoto watapata fursa ya kucheza kandanda, kutengeneza bidhaa za sanaa ya mikono na uchoraji.