Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Takriban 30,000 wakimbilia Uganda kufuatia mapigano ya Juba

Takriban 30,000 wakimbilia Uganda kufuatia mapigano ya Juba

Baada ya serikali ya Sudan Kusini kufungua mipaka yake kwa wanaotoroka mapigano nchini humo, takribani wakimbizi elfu the lathini wamepokelewa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR, na wadau wake nchini Uganda. John Kibego na maelezo zaidi.

(Taarifa ya Kibego)

UNHCR, inasema  watu 24,321 waliingia Uganda kupitia mipaka ya Oraba, Elegu, Lamwo na Moyo, katika siku sita zilizofuata kufunguliwa kwa mipaka, na kwamba asilimia tisini yao ni wanawake na watoto.

Ilipofikia Ijumma wiki jana, jumla ya wakimbizi 26,468 walikuwa wametorokewa Uganda tangu kuibuka kwa mzozo wa kijeshi, tarehe saba mwezi huu jijini Juba.

Baadhi ya wanaosaka hifadhi wanadai kukimbia visa vya uporaji na wavulana kulazimishwa kujiunga na vikundi vya wapiganaji hasa katika maeneo ya Magwi, Jimbo la Eastern Equatoria.

Nimezungmuza na Solomon Isakan, Afisa wa serikali anayehusika na wakimbizi katika ofisi ya Arua

(Sauti ya Osakan)