Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Umoja wa Mataifa wasisitiza manufaa ya yoga

Umoja wa Mataifa wasisitiza manufaa ya yoga

Leo ikiwa ni Siku ya Kimataifa ya Yoga, Katibu Mkuu Ban Ki-moon amesema zoezi hili lenye asili ya kihindi linasaidia kuendeleza heshima kwa binadamu wote na sayari ya dunia. Taarifa zaidi na Priscilla Lecomte.

(Taarifa ya Priscilla)

Kwenye ujumbe wake kwa siku hiyo, Bwana Ban amesema yoga ni aina ya mazoezi ambayo yanaleta afya ya mwili na ya akili pamoja na amani baina ya watu.

Aidha amemulika umuhimu wa maisha yenye afya kwa utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu.

Akizungumza kwa niaba yake kwenye hafla iliyofanyika mjini New York Marekani, msaidizi wa Katibu Mkuu Vijay Nambiar ameeleza manufaa mengi ya yoga.

(Sauti ya Bwana Nambiar)

"Ukosefu wa mazoezi unahusiana na baadhi ya magonjwa yasiyoambukiza, kama vile saratani, kisukari, na magonjwa ya moyo, ambayo ni sababu za kwanza za ugonjwa na vifo duniani kote. Ikiimarisha uzima wa afya, kutufundisha kupumua vizuri na kujitahidi kupunguza msongo wa mawazo yoga inaweza kusaidia kukuza aina za maisha zenye afya zaidi."