Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ICC yamkatia kifungo cha miaka 18 jela Jean-Pierre Bemba

ICC yamkatia kifungo cha miaka 18 jela Jean-Pierre Bemba

Leo juni 21 mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC imemhukumu kifungo cha miaka 18 jela aliyewahi kuwa Naibu Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC Jean-Pierre Bemba Gombo kwa makosa aliyofanya Jamhuri ya Afrika ya Kati. Flora Nducha na taarifa kamili

(TAARIFA YA FLORA)

Machi 21 mwaka huu Bemba alikutwa na hatia kama kamanda wa jeshi ya kutekeleza makosa mawili ya uhalifu dhidi ya ubinadamu, ambayo ni mauaji na ubakaji, makossa matatu ya uhafifu wa vita uyakijumuisha mauaji, ubakaji na uporaji.

Makosa hayo yalitekelezwa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati ya mwezi Oktoba mwaka 2002 na Machi 2003. Nathan Quick ni wakili katika mahakama ICC akisoma hukumu hiyo amesema.

(SAUTI YA NATHAN QUIK)

"Bwana Bemba amehukumiwa kama ifuatavyo: mauaji kama uhalifu wa kivita kifungo cha miaka 16, mauji kama uhalifu dhidi ya aubindamu kifungo cha miaka 16, ukatili wa kingono kama silaha ya vita miaka 18 na wizi wa mabavu kama silaha ya vita kifungo cha miaka 16. Mahakama imeamua kwamba vifungo vyote vitaenda sambamba na kifungo cha juu zaidi cha ukatili wa kingono cha miaka 18."

Muda wote aliokuwa kizuizini tangu 24 Mai 2008 utapunguzwa kutoka kwenye kifungo hicho na mawakili wake wanaweza kukata rufaa ya hukumu hiyo.