Vijana wanahisi tumepotea, hatujali utu- Ban

23 Mei 2016

Mkutano wa kwanza kabisa kufanyika ukiangazia mahitaji ya kibinadamu umeanza hii leo huko Istanbul Uturuki, wakati ambapo mahitaji ya kibinadamu yanaongezeka kila uchao kutokana na majanga asili sambamba na mizozo maeneo mbali mbali duniani. John Kibego na ripoti kamili.

(Taarifa ya Kibego)

Akifungua mkutano huo wa siku mbili Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema zaidi ya watu Milioni 130 wanahitaji misaada kutokana na majanga hayo huku usaidizi ukisuasua na kwamba..

(Sauti ya Ban)

“Nawasihi mdhamirie kupunguza kwa nusu idadi ya wakimbizi wa ndani ifikapo mwaka 2030 na kusaka suluhu bora na za kudumu kwa wakimbizi na waliofurushwa makwao, kwa kuzingatia wajibu wa pamoja.”

 Kwa mantiki hiyo akasema..

“Tuko hapa kuamua mustakhbali tofauti. Leo tunaazimia sisi ni binadamu wamoja tunaowajibika pamoja. Na hebu tuazimie hapa na sasa siyo tu kuwezesha watu kuishi bali pia tuwapatie fursa ya maisha yenye utu.”

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter