Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uteketezaji wa pembe za tembo ni ujumbe wa vita dhidi ya ujangili-Kenya

Uteketezaji wa pembe za tembo ni ujumbe wa vita dhidi ya ujangili-Kenya

Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa, UNDP limetangaza kuanzishwa kwa programu itakayogharimu dola milioni 60 kwa ajili ya kukabiliana na changamoto zinazokabili mazingira na kuangazia uhifadhi wake.

Moja ya sehemu ya mazingira ni wanyama pori amabao hutegemewa kwa ajili ya kuletea nchi kipato kutokana na utalii. Licha ya mchango mkubwa wa wanyama pori lakini mara nyingi ujangili yao unawatia mashakani.

Katika jitihada za kukabiliana na ujangili huo dhidi ya wanyama pori kumefanyika tukio maalum la kuteketeza pembe za ndivu huko Nairobi Kenya. Ungana na Joshua Mmali kwenye makala hii kupata hali halisi.