Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Migogoro inaongezeka juhudi zinahitajika: Ban

Migogoro inaongezeka juhudi zinahitajika: Ban

Mjadala kuhusu mapitio ya operesheni za amani za Umoja wa Mataifa umefanyika hii leo mjini New York ambapo viongozi kadhaa akiwamo Katibu Mkuu Ban Ki-moon wamehutubia hadhira hiyo na kusisitiza umuhimu wa kusongesha mbele operesheni za amani kwa misingi ya maadili.

Katibu Mkuu Ban amesema changamoto ya machafuko imeongezeka mara tatu kwa kipindi cha miaka kumi iliyopita hususani vita vya wenyewe kwa wenyewe na akasema migogoro imekuwa migumu kusuluhisha kutokana na kuvuka mipaka.

Katika juhudi za kusaka suluhu Ban amezungumzia ripoti ya jopo la ngazi ya juu na huru la operesheni za amani pamoja na maazimio kuhusu wanawake,amani na usalama akisema.

( SAUTI BAN)

‘‘Changamoto yetu ni kufanya maazimio haya yawe halisi. Hilo ni jukumu langu kama Katibu Mkuu. Ni jukumu lenu nchi wanachama na wadau, nchi jirani zinazohifadhi wakimbizi, nchiwanachama wa baraza la usalama na kama wachangiaji wa vikosi, polisi na fedha.’’