Vijana wanaweza kutekeleza SDGS wakijumuishwa: Ripoti

28 Machi 2016

Kuwekeza kwa vijana sio tu katika mustakabli lakini pia katika umuhimu wa utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu SDGS, imesema ripoti mya ya Umoja wa Mataifa  kuhusu nafasi ya vijana katika utekelezaji wa SDGS.

Ripoti hiyo ya kwanza imelenga ukanda wa Asia na Pacific ikiitwa Fungua, Vijana katika moyo wa SDGs imezunduliwa leo na msaidizi wa Katibu Mkuu aliye pia Katibu Mtendaji wa kamisheni ya uchumi na kijamii katika ukanda wa Pacific na Asia Dk Shamshad Akhtar.

Licha ya kuonyesha nafasi ya vijana katika utekelezaji wa SDGS kutokana na wingi wao katika ukanda huo, ripoti pia imesema vijana wanakabiliwa na vikwazo katika utekelezaji wa maelengo ya maendeleo endelevu.

Ripoti imesema kuwa kupitia ujumuishwaji na mchakato wa ushirikishwaji ukanda wa Asia na Pacific unaweza kufanikiwa kukabiliana na njaa, changamoto za kiafya, elimu na ukosefu wa ajira kwa kuongeza ujumuishwaji wa kisiasa kwa vijana.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter