Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hatma ya wanyama pori iko mikononi mwetu :UM

Hatma ya wanyama pori iko mikononi mwetu :UM

Kila mwaka Machi 3 ni siku ya kimataifa ya wanyama pori iliyotengwa maalum na Umoja wa mataifa. Mwaka huu kauli mbiu ni “hatma ya wanyama pori ipio mikoni mwetu” ikijikita zaidi katika mustakhbali wa tembo walioko katika orodha ya viumbe vilivyo katika hatari ya kutoweka. Taarifa kamili Flora Nducha

(TAARIFA YA FLORA)

Katika kuadhimisha siku hii Umoja wa mataifa , serikali za Gabon, Ujerumani na Thailand zimeandaa mjadala wa ngazi ya juu hapa makao makuu , kuhusu uhalifu wa kimataifa dhidi ya wanyama pori, wakizishirikisha asasi za kiraia.

Nchini Uganda Mwenyekiti wa kamati ya rasilimali asili walayani Hoima Jackson Mlindambura ameimbia idhaa hii kuwa uwepo wa makazi ya watu sehemu za mbuga na shughuli za kibinadmu ni hatari kwa uwepo wa viumbe hao.

(SAUTI ya JACKSON)

Nayo Tanzania imearifiwa kupoteza asilimia 60 ya tembo wake katika miaka mitano iliyopita hasa kutokana na biashara haramu ya pembe za ndovu, kama anavyofafanua John Scanlon, katibu mkuu wa mkataba wa kiamataifa wa biashara ya viumbe vilivyo katiak hatari ya kutoweka CITES .

(SAUTI YA JOHN SCANLON)

"Tunaamini kwamba hii imekuwa ikichochea sekta ya ujangili na biashara haramu ya pembe za ndovu lakini kuna kazi inaendelea katika nchi zinakotoka, kupitia na hadi zinakokwendana ili kukomesha biashara hii haramu. Na tunaona hatua kubwa ya ushirikiano ili kuhakikisha tunaweza kupunguza kasi ya shughuli za ujangili".