Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban amteua Jen. Balla Keïta wa Senegal kuwa kamanda wa vikosi vya MINUSCA

Ban amteua Jen. Balla Keïta wa Senegal kuwa kamanda wa vikosi vya MINUSCA

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, ametangaza leo kuwa amemteua Luteni Jenerali Balla Keïta wa Senegal kuwa Kamanda wa askari wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR, (MINUSCA).

Luteni Jenerali Keïta anamrithi Meja Jenerali Martin Chomu Tumenta wa Cameroon, ambaye alifariki dunia mnamo Novemba 30, 2015.

Taarifa ya msemaji wake imesema Katibu Mkuu alihuzunishwa sana na kifo cha Meja Jenerali Tumenta, akikariri shukrani zake kwa mchango wake kwa kazi ya Umoja wa Mataifa.

Luteni Jenerali Keïta ana uzoefu wa zaidi ya miaka 40 katika huduma za jeshi kitaifa na kimataifa, na amekuwa Kaimu Kamanda wa MINUSCA tangu Novemba 7, 2015.