Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wagonjwa wa saratani kuongezeka duniani- WHO

Wagonjwa wa saratani kuongezeka duniani- WHO

Kuelekea siku ya saratani duniani hapo kesho ujumbe ukiwa Twaweza, Naweza! Shirika la afya ulimwenguni WHO limekadiria kuongeza kwa wagonjwa kutoka Milioni 14 hadi Milioni 22 miongo miwili ijayo. Flora Nducha na maelezo zaidi.

(Taarifa ya Flora)

WHO inasema ongezeko hilo linachagizwa na kubadilika kwa mfumo wa maisha ikiwemo ulaji chakula kisicho na lishe hasa katika nchi zenye kipato cha wastani na cha chini.

Uvutaji sigara nao unatajwa, halikadhalika ongezeko la idadi ya wazee.

Dokta Ophira ni Mtaalam wa Saratani WHO, na anasisitiza namna jamii inaweza kupunguza mzigo wa ugonjwa huo..

(Sauti ya Ohpira)

“Kwa kutumia mbinu tofauti kwa wakati mmoja, tunaweza kuzuia saratani za aina nyingi, kwa kuchunguza mapema na kutoa matibabu bora, kwa wakati muafaka, na ya bei nafuu. Pia tunaweza kuboresha maisha ya watu wanaoishi na Saratani na hii itapunguzua mzigo mkubwa sana kwa watu na familia zao”