Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

FAO yatia msukumo wa kudhibiti magonjwa kama Ebola na MERS

FAO yatia msukumo wa kudhibiti magonjwa kama Ebola na MERS

Tishio la maradhi ya kuambukiza kwa wanyama kama Ebola na virusi vya corona vinavyosababisha matatizo ya kupumua MERS ni maradhi ambayo yataendelea kuwepo amesema Juan Lubroth, mkuu wa mifugo wa shirika la Umoja wa mataifa la chakula na kilomo FAO, akihoji endapo dunia iko tayari kuyachunguza na kuzuia kuenea kwake.

Ameongeza kuwa cha kutia uchungu Zaidi huenda maradhi hayo yakasambaa au kukazuka tishio la maradhi mengine mapya siku za usoni.

Kwa mujibu wa FAO ili kuyatathimini vyema na kukabili athari zake siku za usoni , watunga sera ni lazima kuendeleza miapngo jumuishi ya utafiti ambayo itatanabisha nini kinajulikana na nini hakijajulikani katika mwenendo wa maambukizi, ili kuimarisha ushirikiano, kushirikiana taarifa na vipimo kama anavyofafanua Dr. Lubroth..

(SAUTI YA JUAN LUBROTH)

"Kuwepo na vipimo vinavyofaa ni muhimu sana, ili kutambua ugonjwa ulipo, na ni ugonjwa gani ,watunga sera wanaweza kuchuka hatua, hatua za kudhibiti maambukizi na kuzuia usambaaji wake."