Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mjumbe wa UM Iraq apongeza ukombozi wa mji wa Ramadi

Mjumbe wa UM Iraq apongeza ukombozi wa mji wa Ramadi

Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu nchini Iraq, Ján Kubiš, ametoa risala za heko kwa watu wa Iraq kufuatia kukombolewa kwa mji wa Ramadi katika mkoa wa Anbar kutoka mikononi mwa kundi la kigaidi linalotaka kuweka dola la Uislamu wenye itikadi kali, ISIS.

Katika taarifa iliyotolewa leo na ujumbe wa Umoja wa Mataifa Iraq, UNAMI, Bwana Kubiš amesema ukombozi huo unaonyesha kuwa ugaidi unaweza, na utashindwa.

Ameongeza kwamba unaonyesha kuwa nguvu za ISIL zimeanza kudidimia taratibu nchini Iraq kwa sababu ya juhudi jasiri na kujitoa kwa vikosi vya usalama vya Iraq, vikosi vya chagizo la umma, Peshmerga na vijana wa makabila ya Iraq.