Ban awa na mazungumzo na Dkt. Elaraby huko Geneva
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon ambaye yuko Geneva Uswisi kwa shughuli kadhaa ikiwemo kushiriki mazungumzo ya kimataifa ya amani kuhusuSyria, amekuwa na mashauriano na Katibu Mkuu wa Umoja wa nchi za kiarabu, Dkt. Nabil Elaraby.
Wawili hao wamejadili mazungumzo ya ngazi ya juu ya kuonyesha mshikamano naSyria yatakayofanyika kesho Jumatano huko Montreaux, na kufuatia na yale ya pande husika kwenye mzozo waSyriayatakayofanyikaGeneva.
Bwana Ban na Dkt.Elaraby wameeleza hofu yao kuhusu athari za mzozo wa Syria huko Mashariki ya Kati hususan nchi jirani na wamejadili suala la huduma za kibinadamu kushindwa kuwafikia walengwa kutokana na mapigano yanayoendelea nchini humo.
Tayari mjumbe wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa nchi za kiarabu Lakhdar Brahimi ametoa taarifa za maandalizi ya mazungumzo ya Geneva.