Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kauli ya mgombea urais Marekani inatishia mpango wa UNHCR:

Kauli ya mgombea urais Marekani inatishia mpango wa UNHCR:

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR limezungumzia kauli iliyotolewa na mmoja wa wagombea urais nchini Marekani ya kutaka waislamu wazuiwe kuingia nchini humo.

Msemaji wa UNHCR, Melissa Flemming akizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva, Uswisi aliulizwa mtazamo wa shirika hilo na kusema..

 (Sauti ya Melissa)

"Tunawasiwasi mkubwa na maneno katika ujumbeunaotumika kwenye kampeni ya uchaguzi Marekani, yanaweka kazi muhimu sana ya uhamiaji hatarini, kazi ambayo inalenga kuwasaidia watu walio katika mazingira magumu na waathirika wa vita ambayo dunia imeshindwa kukomesha, na itakuwa ni aibu ikiwa itasimamishwa, wakati huu ambapo tunahitaji dunia kusimama nasi".

Amesisitiza kuwa Marekani inaongoza duniani kwa kuchukua wakimbizi wengi zaidi na mpango huo hufuatia uchunguzi wa kina wa wakimbizi hao ambao hufanyika kwa takribani miaka miwili kupitia taasisi mbali mbali.