Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mabunge na dhima katika kutekeleza makubaliano ya COP21

Mabunge na dhima katika kutekeleza makubaliano ya COP21

Akiwa jijiini Paris, Ufaransa kwenye mkutano wa 21 wa nchi wanachama wa mkataba wa mabadiliko ya tabianchi, COP21, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema wabunge wana nafasi muhimu katika kuunga mkono utekelezaji wa makubaliano yatakayopitishwa.

Akihutubia spika wa mabunge kutoka nchi wanachama wa mkataba huo, Ban amesema huu ni wakati wa mabunge kuonyesha uongozi wake katika kukabili na kuhimili mabadiliko ya tabianchini.

Amesema wabunge wana nafasi muhimu katika kutafsiri ahadi za kimataifa ili ziweze kuwa na maana na kutekelezeka katika nchi husika

Mathalani amesema mwaka 2009 kulikuwepo na sheria na sera 400 kuhusiana na tabianchi lakini mwaka jana zimeongezeka na kuwa zaidi ya 800 akisema ni matarajio yake kuwa mabunge yatakuwa hima kuchochea mabadiliko ili kujenga dunia ambayo ni salama na yenye ustawi kwa wote.