Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nchi zimechukua hatua kukabiliana na uvuvi haramu-FAO

@FAO/F. Cardia

Nchi zimechukua hatua kukabiliana na uvuvi haramu-FAO

Kuna ripoti kuwa nchi kadhaa duniani zimeanza kuchukua hatua za haraka kukabiliana na uvuvi haramu wa samaki ambao umekuwa ukifanyika sehemu nyingi.

Nchi hizo zimekuwa zikifanya jitihada za makusudi kukabiliana na hali hiyo na huenda hatua hiyo ikapata msukumo mpya kutokana na kuidhinishwa kwa mkakati mpya ambao unazitaka nchi dunia kuwajibika zaidi kukabiliana na ongezeko la meli zinazoranda randa baharini kuendesha uvuvi haramu.

Pamoja na kwamba mkakati huo mpya ni wa hiari lakini kuninishwa kwake na nchi ambazo ni wanachama wa Shirika la chakula na kilimo FAO ni ishara kwamba utekelezaji wake hautakabiliwa na vikwazo.

Mkakati huo umepitishwa leo mjini Roma ambako kunafanyika kongaano la kimataifa lililoandaliwa na kamati maalumu ya FAO.