Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Utumishi wa umma wenye tija ni msingi wa kufikia malengo ya 2015:Ban

UN Photo.
Katibu Mkuu Ban Ki-moon. Picha@

Utumishi wa umma wenye tija ni msingi wa kufikia malengo ya 2015:Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa  Ban Ki Moon leo amesema wakati huu wa changamoto kubwa zaidi duniani zinazotegemeana, utumishi uongozi ulio fanisi na utumishi wa  umma wenye tija ni mambo ya msingi katika kufikia malengo ya maendeleo ya milenia mwaka 2015.

Kauli hiyo ya Ban imo kwenye ujumbe wake wa siku ya utumishi wa umma duniani tarehe 23 Juni inayoangazia kazi muhimu zinazofanywa na watumishi wa umma ili kuboresha maisha ya watu duniani kote.

Maadhimisho yamefanyikaSeoul,KoreaKusini yakishuhudia mashirika 19 ya umma kutoka nchi 14 yakipatiwa tuzo kwa kazi zao bora.

Ban amesema washindi hao wa tuzo wemeendelea kuboresha sekta ya elimu kwa watu wasiobahatika kusoma, wameweka uwazi na uwajibikaji, wametunza na kulinda mazingira,  na pia matumizi ya teknolojia kama mbinu ya kuboresha huduma zao za afya na utoaji wa maji zafi kwa raia.

Katibu Mkuu amesema mwenendo huo wa kasi umeleta manufaa mengi katika utoaji wa huduma za umma kwa wananchi.

Ban amewapongeza washindi kwa kazi na ushupavu  wao na kutaka wafanyakazi wengine wa umma kujifunza kutoka kwao.